Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza wakati wa Mkutano wa pamoja kati yake Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Mark Simmonds (waliokaa kushoto), Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb.) (waliokaa katikati) na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Julai, 2014. Wakati wa Mkutano huo Mawaziri hao waliwaeleza waandishi wa habari masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza ikiwemo Vita dhidi ya Ujangili wa Wanyamapori hususan Tembo na Faru na namna ya kukomesha biashara ya meno ya tembo duniani, Uingereza kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za Kilimo, Mafuta na Gesi, Nishati endelevu na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara. Bw. Simmonds alifanya ziara ya siku mbili nchini kuanzia tarehe 8 hadi 9 Julai, 2014.
|
Mhe. Simmonds nae akiongea wakati wa mkutano huo na Waandishi wa Habari juu ya ziara yake
|
Waziri Nyalandu akizungumza na waandishi wa |
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mawaziri (hawapo pichani) |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.