Mwanamfalme Akishino |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwanamfalme
Akishino wa Japan na Mkewe wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 02 Julai, 2014
kwa ziara rasmi ya siku tano.
Akiwa hapa nchini Mwanamfalme Akishino
atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kutembelea Kituo cha Mafunzo cha Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO); Makumbusho ya Taifa na Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Akiendelea na ziara yake, Mwanamfalme
Akishino atatembelea Visiwa vya Zanzibar na kufanya mazungumzo na Mhe. Dkt. Ali
Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kutembelea eneo
la Mji Mkongwe na hatimaye kuelekea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na
Mbuga ya Wanyama ya Serengeti.
Aidha, katika siku ya mwisho ya ziara
yake Mwanamfalme Akishino atatembelea Banda la Japan kwenye Maonesho ya
Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba.
Mwanamfalme Akishino ambae ni mtoto wa
pili kati ya watoto watatu wa Mfalme Akihito anatarajiwa kumaliza ziara yake
hapa nchini tarehe 06 Julai, 2014 na kuondoka siku hiyo hiyo kurejea nchini
kwake.
IMETOLEWA
NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
01
JULAI, 2014
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.