TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya
hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat,
amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya
ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa Saba mchana ofisini
kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Lbya.
Inataarifiwa kuwa Bwana
Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.
Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta
Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini. Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay
ambako alitangazwa kuwa alikwisha kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho.
Maiti imehamishiwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.
IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam
Julai 2,2014

No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.