Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiongea jambo wakati alipokutana na wawakilishi wa nchi za G4 hapa nchini ambazo ni India, Brazil, Ujerumani na Japan. Mwingine katika picha ni Bibi Ramla Khamis, Afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje. Balozi Mushy na wawakilishi hao walijadili masuala ya mabadiliko katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo alisisitiza msimamo wa bara la Afrika wa kupatiwa nafasi mbili za ujumbe wa kudumu zenye kura ya turufu katika Baraza hilo pamoja na nafasi tano za ujumbe usio wa kudumu. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.