Friday, February 27, 2015

Naibu Katibu Mtendaji wa ICGLR atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

Kaimu Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha akizungumza na Naibu Katibu Mtendaji Mhe. Vicente Mwanda wa Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR), alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Bwa. Innocent Shiyo (Wa kwanza Kushoto), katikati ni Afisa Mambo ya Nje Bi. Grace Martin, na wakwanja kulia ni Bwa. Ally Ubwa Afisa Mambo ya Nje wakiwa katika mazungumzo hayo kati ya Balozi Gamaha na Bwa.Vicente Mwanda (Hawapo pichani) 

Bwa. Robert Simukoko afisa aliyeambatana na Naibu Katibu Mtendaji

Picha na Reginald Philip

Rais Kikwete akutana na Watanzania waishio Zambia


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Jumuiya ya Watanzania waishio Zambia (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi nchini humo kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Edgar Chagwa Lungu.
Sehemu ya Jumuiya ya Watanzania waishio Zambia wakimsikiliza Rais Kikwete (hayupo pichani) alipozungumza nao.

Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Juma Maharage (wa pili kushoto) akiwa na Balozi Samwel Shelukindo (wa pili kulia), Mshauri wa Rais Masuala ya Diplomasia pamoja na Bi. Zuhura Bundala (kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Talha Mohammed (kusoto) Afisa Mambo ya Nje wakimsikiliza Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani alipozungumza na Diaspora ya Zambia
Sehemu nyingine ya Watanzania hao wakishangilia hotuba ya Mhe Rais
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akijibu moja ya maswali wakatiwa Mkutano wa Rais Kikwete na Watanzania waishio Zambia. Wengine ni Mama Salma Kikwete, Waziri wa Fedha, Mhe. Saaada Mkuya Salu na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro 


Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma naye akizungumza wakati wa mkutano huo
Rais Kikwete akiagana na Watanzania hao mara baada ya kuzungumza nao
Mama Salma Kikwete akipata picha na baadhi ya Watanzania waishio Zambia
==================================



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewahimiza Watanzania wanaoishi nje ya nchi kujenga nyumbani, kuwa waadilifu na kuishi kwa  kufuata sheria za nchi walizopo.

Rais Kikwete alitoa rai hiyo wakati wa mkutano wake na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Zambia wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya nchini humo  hivi karibuni.

Mhe. Rais Kikwete ambaye alizungumzia masuala mbalimbali yanayoendelea nchini ikiwemo hali ya siasa, uchumi, elimu na miundombinu kwa Jumuiya hiyo alisema kuwa, imefika wakati sasa kwa Watanzania wanaoishi nje kuzisaidia jamii zao zilizobaki nchini hususan katika suala la elimu ili kuziinua.

 “Nawahimiza ndugu zangu jengeni nyumbani, heshima ya mwanadamu ni kupata mahali pa kukaa pia inapowezekana saidieni ndugu zenu hususan katika elimu ili nao waimarike”, alisisitiza Rais Kikwete.

Pia Mhe. Rais aliwaasa kuheshimu sheria za nchi walizopo kwa kuzingatia maadili na kusisitiza kuwa sheria haibadiliki iwe ni ndani ya nchi au nje hivyo ni wajibu wao  kuzifuata sheria zilizowekwa ili waishi kwa amani na kufanya shughuli zao.

Akizungumzia masuala ya uchumi nchini alisema kuwa hali ni nzuri  ambapo mfumuko wa bei unaendelea kupungua na pia hali ya chakula ni nzuri na kwamba Serikali inajaribu kutafuta masoko kwa chakula cha ziada.

“Hadi sasa kuna tani laki 6 za mchele na mahindi tani milioni 2.6 ambazo ni ziada. Hivyo kazi kubwa sasa ni kuangalia masoko na pia namna ya kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye” alisema Rais Kikwete.

Kuhusu elimu, Mhe. Rais Kikwete alisema kuwa Serikali imefanikiwa kuwawezesha watoto wote wanaofaulu kwenda Sekondari pia wale wanaotakiwa kujiunga na darasa la kwanza wanajiunga. 

Alisema Serikali imejenga Sekondari za kutosha ambapo alitoa mfano wa Wilaya ya Kinondoni ya Jijini Dar es Salaam kuwa mwaka 2006 ilikuwa na Sekondari za Serikali 5 pekee lakini hadi kufikia mwaka 2014 kuna jumla ya Sekondari 49. Aidha, wanafunzi waliofaulu na kujiunga na Sekondari hizo Wilayani humo ni Milioni 1.9 kutoka laki 525 mwaka 2005.

“Tumepiga hatua kubwa sana katika suala la elimu, tumejenga Sekondari za kutosha na maabara na sasa tunajitahidi kutafuta vitabu na walimu wa masomo ya sayansi ili kukidhi haja ya masomo hayo nchini”, alifafanua Rais Kikwete.

Mhe. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuipongeza Jumuiya hiyo yenye zaidi ya Watanzania mia tatu kwa kuanzisha chama na kuwataka wakitumie kama jukwaa la kuwaunganisha na kuwasiliana.  

Awali akijibu swali kuhusu  uraia pacha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe alisema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje imeendelea na jitihada za kutambua Watanzania wote walioko nje ya nchi (Diaspora) lakini pia suala hilo lilipelekwa na kujadiliwa na Tume ya Katiba.

“Kama Wizara tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Watanzania wote walioko nje ya nchi wanatambulika lakini pia tumehakikisha Katiba inayopendekezwa ina kipengele kinachohusu diaspora. Kipengele hicho kinanaeleza kuwa Mtanzania aliyeko nje ya nchi (diaspora) anaweza kupata haki kadhaa sawa na raia kwa kupewa hadhi maalum”, alifafanua Waziri Membe.

Rais Kikwete ambaye alikuwa nchini humo kwa mwaliko wa Rais wan chi hiyo Mhe. Edgar Chagwa Lungu alifuatana na Mama Salma Kikwete, Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia na Viongozi Waandamizi kutoka Serikalini na Mamlaka mbalimbali.

_Mwisho_


Thursday, February 26, 2015

Naibu Waziri Azindua Kitabu kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Maadhi Juma Maalim akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu chake "The United Republic of Tanzania in the East African Community, Legal Challenges in Integrating ZanzibarKitabu hicho  kinazungumzia nafasi ya Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na na ndani ya Africa Mashariki,  muundo wa muungano, chanagamoto na mafanikio na hatimaye kuelekea kwenye shirikisho la Afrika Mashariki. 
Prof. Gordon Woodman (wa kwanza kushoto), katikati ni Prof. Josephat L. Kanywanyi, wa kwanza kulia ni Dkt.Mapunda wakimsikiliza Dkt. Maadhi akitoa maelezo ya ufafanuzi kuhusu kitabu hicho.


Sehemu ya wageni waliohudhuria Hafla hiyo

Picha ya Pamoja
Naibu Waziri Dkt. Maadhi akipongezwa na  Jan-Dieter Gosink kutoka Ubalozi wa Ujurumani Nchini Tanzania
Dkt. Maadhi Juma Maalim akiwa katika picha ya Pamoja na Prof Woodman katika hafla ya uzinduzi wa kitabu.
Mhe. Dkt.Mahadhi akisalimiana na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Prof. Wanitzek akiwaeleza jambo Pro. Josephat L. Mnywanyi pamoja na Dkt. Mongela
 Prof. Bonaventure Rutinwa (pili kulia) akifurahia uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na Dkt. Maadhi Juma Maalim ( pili kutoka Kushoto) pamoja na Dkt. Mongela ( kwanza kutoka kushoto), katikati ni Prof. Wanitzek, na wakwanza kulia ni Dkt. Mapunda
Dkt. MaadhiJuma Maalim akimsikiliza Dkt. Lilian Mihayo Mongela, wa kwanza kulia ni Dkt. Anatole Nahayo
Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Wakwanza kulia), Dkt. Anatole Nahayo (Wa Kwanza Kushoto) na Katikati ni Dkt. Lilian Mihayo Mongela wakiwa katika Picha ya Pamoja na Vitabu vitabu walivyoandika.

Picha na Reginald Philip

Naibu Waziri Mambo ya Nje amuaga Balozi wa Japan

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akisalimiana na Balozi wa Japani anayemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Masaki Okada wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akibadilishana mawazo na Mhe.Masaki Okada, Balozi wa Japani anayemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Katikati ni mke wa Balozi Mama Okada.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Dkt.Mahadhi Juma Maalim (Mb) akisoma hotuba wakati wa hafla hiyo.
 Mheshimiwa Naibu Waziri akiendelea na hotuba huku wageni waalikwa wakimsikiliza.
 Balozi wa Japani anayemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Masaki Okada na Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wakiwa wamenyanyua glasi zao juu kabla ya kugongeana glasi kwa ajili ya kutakiana heri na afya njema.
 Wageni waalikwa nao wakifanya ishara ya kutakiana heri katika hafla hiyo.
 Balozi wa Japani anayemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini Mhe. Masaki Okada akitoa shukrani zake kwa ushirikiano mzuri alioupata akiwa nchini Tanzania.
 Naibu Waziri Mhe.Mahadhi Juma Maalim (kulia), Balozi Mbelwa Kairuki (katikati), Mkuu wa Idara ya Asia na Australasia na Bibi Rosemary Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wakimsikiliza Balozi Masaki Okada kwa makini  katika hafla hiyo
 Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Okada kwa makini.
  Bw. Adam Issara, Msaidizi wa Naibu Waziri (kulia) Bi.Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali (katikati) na Mke wa Balozi Mama Okada wakifuatilia kwa makini shukrani za Mhe. Balozi Okada.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) akimkabidhi zawadi Mhe. Balozi Okada katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

Rais Kikwete ashiriki Dhifa ya Kitaifa wakati wa ziara yake nchini Zambia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa kwanza wa Zambia, Mhe. Keneth Kaunda mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Taj  Pamodzi kwa ajili ya kushiriki Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima  yake  na Rais Edgar Lungu wa Zambia (mwenye tai ndogo nyeusi). Mhe. Rais Kikwete amefanya ziara ya siku mbili nchini Zambia kwa mwaliko wa Rais Lungu.
Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Lungu pamoja na Wake zao Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba chekundu) na Mama Esther Lungu (wa kwanza kulia) wakifuatilia sala iliyotolewa kabla ya kuanza kwa Dhifa hiyo. Wengine ni Rais Mstaafu wa Zambia, Mhe. Kaunda, Makamu wa Rais wa Zambia, Bibi Inonge Wina (watatu kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
Rais Lungu akitoa hotuba
Viongozi wakitakiana afya njema na kuimarisha ushirikiano 
Mhe. Kaunda, Mhe. Wina na Mhe. Membe wakitakiana afya njema
Rais Kikwete akitoa hotuba

Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya pamoja na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Charles Tizeba nao wakishiriki dhifa hiyo
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma (kushoto) akiwa na Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mhe. Judith Kapijimpanga wakati wa dhifa
Mkuu wa Moa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Salva Rweyemamu na Bw. Togolani Mavura wakati wa dhifa.
Sehemu ya Wageni waalikwa
Wageni waalikwa
Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Kaunda wakitakiana afya njema
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania
Ujumbe wa Tanzania