Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati)
akimsalimia Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,jijini
New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakati Waziri huyo
alipowasili ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo katika Jiji la Washington
DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu
na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati),
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula
(kushoto)na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, jijini New York, nchini humo, Tuvako Manongi wakiwa katika
picha ya pamoja mara baada ya kumpokea Waziri huyo aliyewasili
jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa
Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho.Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. | |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.