Wednesday, February 4, 2015

Matukio mbalimbali ya ziara ya Rais wa Ujerumani nchini


...Mkutano na Waandishi wa Habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck wakati wa Mkutano wa Pamoja na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) uliofanyika Ikulu Dar es Salaam kuelezea malengo na mafanikio ya ziara ya Rais Gauck  hapa nchini.
Sehemu ya Wajumbe kutoka Ujerumani na Tanzania pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Mhe. Rais Kikwete  akiongozana na Rais Gauck mara baada ya mkutano wao na waandishi wa habari

....Dhifa ya Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck pamoja na Mama Salma Kikwete na Mama Schadt, Mke wa Rais wa Ujerumani wakati wa Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa Ikulu, Dar es Salaam kwa heshima ya Rais Gauck. Rais Gauck yupo nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku tano.
Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Gauck wakitakiana afya njema na ushirikiano imara baina ya nchi zao wakati wa dhifa hiyo huku Mama Salma akishuhudia.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal pamoja na Mke wake Mama Asha Bilal (mwenye kilemba) wakijadili jambo na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Diana Melrose wakati wa dhifa ya kitaifa Ikulu. Kulia ni Mkurugenzi wa EPZA Kanali Mstaafu, Joseph Simbakalia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiteta jambo na mmoja wa wajumbe waliofuatana na Rais wa Ujerumani waliposhiriki dhifa ya kitaifa Ikulu
Dhifa ikiendelea
Brass Band ikitumbuiza wakati wa dhifa hiyo
Rais Gauck na Mke wake Mama Schadt wakifurahia burudani ya ngoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (katikati) akimsikiliza mmoja wa wajumbe waliofuatana na Rais Gauck walipokuwa wakati wa dhifa ya kitaifa iliyofanyika Ikulu
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Sophia Mjema akifafanua jambo kwa Balozi Melrose huku Bibi Victoria Mwakasege, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisikiliza
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimweleza jambo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizarani hapo, Bi. Mindi Kasiga huku Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizarani hapo akisiskiliza.

Picha na Reginald Philip














No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.