Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Wakuu wa Nchi zinazounda Ukanda wa Kati yaani Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ufunguzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam ulihudhuriwa na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza na Mawaziri waliowawakilisha Marais wa DRC na Rwanda. Pamoja na mambo mengine mkutano huo ulijadili umuhimu wakuendelea kuimarisha miundombinu ya nchi za Kanda ya Kati hususan barabara, reli na bandari ili kukuza uwekezaji na maendeleo kwa ujumla. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.