Tuesday, April 28, 2015

Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Japan.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Japan hapa nchini Mhe.Masaharu Yoshida. Hafla hiyo fupi ilifanyika Wizarani tarehe 28 Aprili, 2015
Balozi Mteule wa Japan hapa nchini Mhe.Masaharu Yoshida akimsikiliza kwa makini Waziri  Membe muda mfupi baada ya kukabidhi nakala zake za hati za utambulisho.
Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Asia na Australasia Bw.Nathaniel Kaaya (mwenye tai nyekundu)  kwa pamoja na Bw.Thobias Makoba, Katibu wa Waziri na Afisa kutoka Ubalozi wa Japan hapa nchini wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Membe na Balozi Yoshida (hawapo pichani)
Kikao kikiendelea.
Waziri Membe akifafanua jambo kwa Balozi Yoshida huku Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi.Mindi Kasiga (kulia) akinukuu mazungumzo hayo.
 Mhe. Yoshida nae akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho huku Mhe. Waziri Membe na Maafisa wakimsikiliza kwa makini.

Waziri Membe akifurahia jambo na mgeni wake Balozi Mteule wa Japan Mhe. Yoshida.
 Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Japan hapa nchini Mhe. Yoshida  mara baada ya kukabidhi nakala zake za hati za utambulisho.

Picha na Reuben Mchome.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.