Rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Robert Mugabe akiangalia Hati Miliki ya Majengo ambayo Serikali ya Zimbabwe imetoa kwa SADC kuwa Kituo cha Kufundishia Walinda Amani. Hati hiyo ilikabidhiwa kwa Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax anayeonekana kushoto. Majengo hayo yapo kwenye kiwanja chenye ukubwa wa ekari 16 ambayo Zimbabwe imetoa bure kwa SADC kama mchango wake wa kuhamasisha amani na utulivu barani Afrika. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.