Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akiwajadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR), Balozi Mwanaidi Maajar huku Mkuu wa Chuo hicho Balozi Mohammed Maundi akisiskiliza wakati viongozi hao wakisubiri kumpokea Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi alipotembelea Chuoni hapo leo tarehe 18 Mei, 2015 wakati akiendelea na ziara yake ya kitaifa ya siku tatu hapa nchini. Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini, Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 1978 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.