Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Awamu ya
Tatu yenye jumla ya Watanzania 39 kutoka Yemen wanatarajiwa kuwasili nchini
tarehe 06 Mei, 2015 ikiwa ni jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuwarejesha nyumbani kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea
nchini humo.
Watanzania
hao wakiwemo Wanafunzi watawasili nchini kwa Ndege ya Shirika la Qatar namba QR
1349 majira ya saa 1.55 (saa moja) asubuhi.
Kurejea
kwa Watanzania hao kutafanya jumla ya Watanzania waliorejea kutoka Yemen hadi
hivi sasa kuwa 62 kati ya Watanzania 69 waliojiandikisha
kurudi huku jitihada za kuwaandikisha wengine zikiendelea
kufanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman.
Awamu ya
kwanza ya Watanzania waliorejea ilihusisha familia ya watu watano huku awamu ya
pili ilikuwa na Watanzania 18.
Itakumbukwa
kuwa, hivi karibuni Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe ilitangaza kuwarejesha nchini
Watanzania waliopo Yemen kufuatia machafuko yanayoendelea nchini humo.
IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO
YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.
05 MEI, 2015
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.