Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akiwakaribisha nchini Timu ya Madaktari kutoka Marekani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni. Madaktari hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa mbalimbali katika Hospitali za Mwananyamala ya Jijini Dar es Salaam na Mnazi Mmoja, Zanzibar. Ziara ya Madaktari hao ambao wametoka Majimbo ya Washington DC, Maryland na Virginia imeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani (Diaspora). |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.