Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka kwa taasisi ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala Nchini Uganda. Pichani ni kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt. Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo, Rais Kikwete pia amepokea tuzo ya kuitambua Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na Utulivu, Huduma bora za kijamii na Maendeleo makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake.
(Picha na Freddy Maro).
=================
=================
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Amani
na utulivu ulioko nchini , umechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wote wa
Tanzania.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo leo Ikulu wakati akipokea nishani ya Amani
kutoka kwa Dr. Paul Bamutize, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya East Africa Book Records yenye makao yake makuu nchini Uganda.
Rais
amepokea nishani mbili leo ambazo ni kwa ajili ya nchi na ingine kwa ajili yake
kama Kiongozi wa Tanzania.
Dr.
Bamutize amesema Tanzania imekua mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki ambapo pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi kama chama ambacho
kimesimamia Amani hiyo hapa nchini.
“Amani
hii tuliyonayo hapa nchini imechangiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa
Tanzania ambao napenda kupokea nishani hii kwa niaba yao kwa sababu wao ndiyo
watunzaji na walinzi wakubwa wa Amani hii”
Rais Kikwete amesema.
Dr.
Bamutize amempongeza Rais Kikwete na kuelezea kuwa amani hiyo imeleta matumaini
kwa wawekezaji na majirani wa Tanzania na hivyo kuwa mfano wa kuigwa na
majirani zake wote katika ukanda huu na Afrika kwa ujumla.
Hafla
hiyo fupi imehudhuriwa na mabalozi wa Burundi, Kenya, Rwanda, Jamhuri ya Watu
wa Congo na Uganda.
Wakati
huo huo Rais Kikwete amepokea Ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa India Mhe.
Narendra Modi.
Ujumbe
huo umeletwa Ikulu na Mheshimiwa Rajiv Pratap Rudy Waziri wa Nchi
anaeshughulikia Maendeleo ya Ujasiriamali ambaye pia amefanya mazungumzo na
Rais Kikwete kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na ushirikiano katika
biashara na ujasiriamali.
……………………………Mwisho……………………………
Imetolewa na :
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-Dsm
8
Septemba, 2015
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.