JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
Taarifa
zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko
makubwa imepokea majina mengine mawili ya Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki dunia
kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah
tarehe 24 Septemba, 2015 na kupelekea vifo vya Watanzania kufuatia tukio hilo
kufikia watu saba (7) hadi sasa.
Majina ya Mahujaji hao ni Bw.
Athumani Mateso Chaulana na Bw.
Ahmed Said Bawazir ambao kupitia picha zao wametambulika kuwa wamefariki
dunia.
Aidha, Wizara imepokea majina mapya 19 ya Mahujaji kutoka Tanzania
ambao bado hawajaonekana. Itakumbukuwa kuwa tarehe 29 Septemba, 2015 Wizara ilitoa
taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji wa Tanzania ambao ni kati ya 50 ambao bado hawajaonekana. Kupatikana kwa
majina hayo kunafanya idadi ya Mahujaji waliopotea na majina yao kutambulika
kufikia 37.
Orodha ya majina mapya 19 ya Mahujaji
wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-
1. Juma Bajuka
2. Masoud Juma
3. Issa Amir Faki
4. Juma Jecha
Dabu
5. Nassor
Mohammed Hemed
6. Mohamed Awadh
Namongo
7. Juma Bakula
8. Said Habib
9. Hamis Juma
Shamte
10.
Khadija
Hamad
11.
Rahma
Salim
12.
Hadija
Abdallah Sefu
13.
Farida
Khamis
14.
Laila
Manunga
15.
Bi.
Hawa Amrani Khamis
16.
Saida
Awadhi
17.
Maimuna
Seleman Ruwaly
18.
Jalia
Kassim Mashule
19.
Nuru
Omar Karama
Mbali na
taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kuonekana Mahujaji
saba wakiwa hai. Mahujaji hao ni:-
1. Ali
Abdulrahman (Abidina)
2. Abdallah
Hassan Pande
3. Suleiman Ali
Kidogoli
4. Mohammed Salum
5. Mwadini Hassan
6. Habiba
Ramadhan Ali (Maulana)
7. Ramadhan
Muhsin
Ubalozi kwa
kushirikiana na Tanzania Hajj Mission
na Vikundi vya Mahujaji unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa
Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi
maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakiki picha za
mahujaji waliofariki ili kubaini Mahujaji kutoka Tanzania.
Wizara
inapenda kufafanua kuwa, orodha inayotolewa si kamili kwa maana kwamba inaweza
kuongezeka kwa vile baadhi ya majina ya Mahujaji yaliwayowasilishwa Ubalozini
na ndugu wa mahujaji waliopotea hayamo katika orodha hii. Pia Ubalozi
unaendelea kuwasiliana na vikundi vilivyopeleka Mahujaji ili kuweza kupata
taarifa kamili na sahihi ya jumla ya Mahujaji wote ambao hawaonekani.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
30 Septemba, 2015
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.