JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
Taarifa
zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko
makubwa imepokea jina la Bw. Khamis Juma
Shamte hujaji kutoka Tanzania aliyefariki dunia kufuatia tukio la
mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba,
2015. Kifo cha Bw. Shamte kinafanya idadi ya vifo vya Watanzania kufuatia tukio
hilo kufikia watu nane (8) hadi sasa.
Aidha, Wizara imepokea jina la Bi
Hawa Amrani Khamis aliyekuwa amepotea tangu siku ya ajali hiyo ambaye
amepatikana akiwa mzima na aliweza kuungana na Mahujaji wengine na kurejea
nyumbani tarehe 02 Oktoba, 2015.
Vile vile orodha ya majina ya majeruhi wote wa ajali ambao bado
wapo hospitali imetolewa. Hadi sasa kuna Mahujaji wanne (4) wa Tanzania ambao
wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali za Saudi Arabia na
hali zao zinaendelea vizuri. Mahujaji hao ni Bi. Hidaya Mchomvu, Bi. Mahjabin Taslim Khan na Bw. Ahmed Abdalla Jusab. Pia, kuna mgonjwa mmoja ambaye aliugua
tangu alipowasili Madina akitokea nchini anayeitwa Mustafa Ali Mchira ambaye bado amelazwa katika Hospitali ya Ansari
Madina katika chumba cha wagonjwa mahututi. Bw. Mchira hakujeruhiwa kwenye
ajali ya mkanyagano.
Hadi kufikia tarehe 03 Oktoba, 2015, Ubalozi wa Tanzania nchini
Saudi Arabia kwa kushirikiana na Tanzania
Hajj Mission na Vikundi vilivyopoteza Mahujaji umefanikiwa kupata majina ya
Watanzania 32 ambao bado hawajapatikana. Orodha ya Majina na Vikundi vyao ni
kama ifuatavyo:-
KIKUNDI CHA KHIDMAT ISLAMIYA
1. Abdul Iddi
Hussein
2. Awadh Saleh
Magram
3. Burhan Nzori
Matata
4. Yussuf Ismail
Yussuf
5. Saleh Mussa
Said
6. Adam Abdul
Adam
7. Archelous
Anatory Rutayulungwa
8. Farida Khatun
Abdulghani
9. Rashida Adam
Abdul
10.
Hamida
Ilyas Ibrahim
11.
Rehema
Ausi Rubbaga
12.
Faiza
Ahmed Omari
13.
Khadija
Abdulkhalik Said
14.
Shabinamu
Ismail Dinmohammed
15.
Salama
Rajabu Mwamba
16.
Johari
Mkesafiri Mwijage
KIKUNDI CHA TCDO
17.
Alwiya
Sharrif Abdallah
18.
Hafsa
Sharrif Saleh Abdallah
KIKUNDI CHA AHLU DAAWA
19.
Masoud
Juma
20.
Issa
Amiri Faki
21.
Juma
Jecha Dabu
22.
Nassor
Mohammed Hemed
23.
Mohammed
Awadh Namongo
24.
Juma
Yussuf Bajuka
25.
Said
Habibu Ferej
26.
Khadija
Hamad
27.
Rahma
Salim
28.
Hadija
Abdallah Sefu
29.
Farida
Khamis
30.
Nuru
Omar Karama
31.
Laila
Manunga
32.
Saida
Awadh
Zoezi la kuwatambua Mahujaji wa Tanzania ambao bado hawajaonekana
linaendelea. Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha nyingine zipatazo elfu moja
(1,000) kwa ajili ya kuangalia Mahujaji waliofariki dunia katika ajali hiyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
05 Oktoba, 2015
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.