Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akizugumza siku ya Alhamis wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likijadili Taarifa ya mwaka ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa. Na Mwandishi Maalum, New York
Tanzania imekaribisha juhudi zinazochuliwa na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa za kuboresha uwazi na utendaji wenye tija wa chombo hicho juhudi ambazo pia zinahusisha mijadala ya wazi.
Hayo yameelezwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilipokuwa likijadili Taarifa ya Mwaka ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Taarifa hiyo iliwasilishwa siku ya alhamisi na Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza, Balozi Matthew Rycroft ambaye nchi yake ndiye Rais wa Baraza Kuu la Usalama kwa mwezi huu wa Novemba.
Taaria hiyo ambayo ni ya kuanzia Agosti Mosi 2014 hadi Julai 31 2015 imeanisha mikutano ya wazi na ya ndani iliyofanywa na Baraza kwa kipindi hicho, maazimio yaliyopitishwa, taarifa za rais wa Baraza kwa mwezi, na ziara za kikazi zilizofanywa na wajumbe wa Baraza. ambaye ni Mwakilishi wa Kudumu wa Uingereza Balozi katika Umoja wa Mataifa.
Balozi Mwinyi, amesema mijadala ya wazi inayoandaliwa na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa inatoa fursa na kufungua milango kwa nchi nyingi zaidi kushiriki nje ya wajumbe 15 wa Baraza na kwamba Tanzania ni kati ya nchi ambazo zimekuwa ikishiriki mijadala hiyo ya wazi.
Pamoja na kupongeza juhudi hizo, Mwakilishi huyo wa Tanzania, amesema, ni matumaini ya Tanzania kuwa katika siku za usoni, Baraza Kuu la litaanda mijadala katika namna ambayo itawezesha wajumbe kuzingatia hoja zilizotolewa na washiriki wengine kabla ya kupitisha matokoe ya mijadala hiyo.
Vilevile Balozi Mwinyi amesema, juhudi zinazochukuliwa na wadau mbalimbali za kudhibiti matumizi ya kura ya turufu hasa katika kuzuia mauaji ya halaiki, ni juhudi sahihi na zinazopashwa kuugwa mkono.
Akizungumzia zaidi matumizi ya kura ya turufu, Balozi Ramadhan Mwinyi ametoa wito kwa mataifa yenye hadhi ya kutumia kura hiyo kuhakikisha kwamba wanaitumia pale tu inapobidi na kwa kuzingatia matakwa na mamlaka zilizoainishwa Katiba ya Umoja wa Mataifa.
“ Tuna toa wito wa Baraza kuu la Usalama la Umoja wa mataifa, kuingiza katika taarifa zake za baadaye kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, tathmini ya matokeo ya maamuzi pale kura ya turufu ilipotumika na matokeo ya pale ambapo kura ya turufu haikutumika katika maamuzi yaliyofikiwa” akasisitiza Balozi Mwinyi.
Kuhusu yaliyomo katika taarifa hiyo, Balozi amesema, Tanzania inaungana na nchi nyingine katika kutaka taarifa hizo ziwe na uchambuzi wa kina na zilizo makini badala ya kuorothesha kazi za Baraza hilo kama ilivyo sasa.
Tanzania pia kupitia Mwakilisihi wake , imekaribisha namna ambavyo Baraza Kuu la Usalama linavyopanua wigo wa majadiliano na Vyombo vingine zikiwamo Asasi za kijamii na wanazuoni katika kujadilia masuala mtambuka.
“ Hata hivyo tumegundua kuwa baadhi ya mada zinazojadiliwa siyo tu zimekuwa zikiwagawa washiriki lakini pia zinakuwa nje ya mamlaka ya Baraza. Tunaomba tukumbushe kwamba Baraza Kuu la Usalama kama Chombo wakilishi cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Baraza linatakiwa kujiepusha mada ambazo hazina tija”.
Baadhi ya wazungumzaji wengine waliochangia taarifa hiyo ya Baraza Kuu la Usalama, wameelezea kwamba licha ya utekelezaji wa mamlaka ya Baraza hilo katika kusimamia Amani na usalama wa kimataifa, Baraza limeshindwa kabisa kumaliza baadhi ya migogoro kama ule wa Syria ambao umedumu kwa muda mrefu. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.