Kutoka kushoto ni Ndg. Shamy Chamicha, Ndg. Jackosn Bulili, Mhe. Balozi Kasyanju,
Ndg. Florence Chakina na Ndg. Hofman Sanga.
Mhe. Irene F. M. Kasyanju, Balozi wa Tanzania, Uholanzi
amekutana na wanafunzi wanne (4) kati ya watano (5) wa Kitanzania wanaosoma shahada
tofauti katika Taasisi iitwayo “International Institute of Social Studies (ISS)”,ya
Chuo Kikuu cha Erasmus, Rotterdam ambao walifika Ubalozini kwa lengo la
kumsalimu na kufahamiana.
Pamoja na mambo mengine wanafunzi hao wamewasilisha ombi
lao kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Mhe. Balozi wa kuiomba
isaidie kuhakikisha kuwa idadi ya “Scholarships” kwa Tanzania kwenye Chuo hicho
inaongezeka. Hii ni kutokana na idadi ya
Watanzania wanojiunga na ISS kupungua sana ukilinganisha na nchi zingine za Afrika
hususan za Afrika Mashariki, tofauti na ilivyokuwa zamani.
Balozi kwa upande wake alipokea ombi lao na kuahidi kulifanyia
kazi ipasavyo. Aliwashukuru wanafunzi hao kwa kufika Ubalozini kujitambulisha na
akawaahidi ushirikiano wakati wote watakaokuwepo Uholanzi.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.