Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Mlima amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa New Zealand nchini mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini Mhe. Richard Mann, katika mazungumzo yao Balozi Mann alitumia fursa hiyo kumpongeza Balozi Mlima kwa uteuzi na aliishukuru Wizara kwa ushirikiano anaoupata katika utendaji utekelezaji wake wa majukumu. Kwa upande wa Balozi Mlima alimweleza kuwa wataendelea kushirikiana vyema na nchi ya New Zealand katika sekta mbalimbali katika kukuza uchumi. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.