Balozi
wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule (kushoto) akizungumza na
Mkurugenzi wa Mashariki mwa Afrika wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya
Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Bw. Jose Vila De-Castillo,
alipotembelea Ubalozini, Jijini Nairobi, jana.
Katika mazungumzo yao, Bw. De-Castillo aliomba
Ubalozi uwe kiungo kati ya Taasisi yake na Serikali ya Tanzania. Taasisi
hiyo inaendesha mpango wa miaka mitano wa udhibiti wa rushwa, mitandao
ya uhalifu, biashara na matumizi ya madawa ya kulevya, ujangili na
biashara ya binadamu kwa nchi za Tanzania, Burundi,Comoro,
Djibouti,
Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles na
Somalia. Kulia ni Ofisa wa Ubalozi, Bw. Mussa Haji.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.