Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Mwinyi akiwa katika mazungumzo
na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (Association of Local Authorities of Tanzania-ALAT),
Bw. Abraham Shamumoyo. Katika mazungumzo hayo, Bw. Shamumoyo alitoa
taarifa fupi kuhusu muundo na utendaji kazi wa ALAT. Aidha, Bw.
Shamumoyo alitoa taarifa za awali kuwa Jumuiya hiyo kwa upande wa Kanda
ya Mashariki mwa Afrika inakusudia kutuma maombi Serikalini ili makao
makuu yake yawe Tanzania. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.