Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini, Dkt. Lu Youqing, alipotembelea Wizarani jana. Katika Mazungumzo yao Balozi huyo wa Jamhuri ya Watu wa China nchini alielezea taratibu zinazofanywa na mamlaka za nchi hiyo katika kutekeleza ahadi zake za miaka mitatu (2016-2018) zilizoahidiwa katika Mkutano wa Sita wa kilele cha Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, ambapo alieleza miradi itakayotekelezwa ni ile ya kuendeleza Viwanda na Ujenzi wa Miundombinu. |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.