MFA Tanzania

Thursday, March 24, 2016

Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje yaitaka Wizara kusimamia Sera ya Diplomasia ya Uchumi

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb)kushoto pamoja na Mwenyekiti  wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Balozi Adadi Rajab wa pili kulia na Makamu wake Mhe. Masoud Ali Khamis wa tatu kulia wakiwa katika kikao cha kamati hiyo kinachofanyika Jijini Dar es salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri Mahiga, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt Susan Kolimba (Mb.) na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Aziz Mlima wakifuatilia kikao hichoambapo kamati ilipokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Wizara. Sambamba na hilo Wajumbe wa kamati hiyo wameitaka wizara kuweka mikakati na kuongeza jitihata zaidi katika kuhakikisha inazitangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini.
 Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia mazungumzo.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge.

 Sehemu ya Wakurugenzi na  Maafisa wa Wizara wakifuatilia kikao.
 Sehemu nyingine ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia kikao


ForeignTanzania at 9:12 AM
Share

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.

‹
›
Home
View web version

About Me

My photo
ForeignTanzania
View my complete profile
Powered by Blogger.