Friday, March 11, 2016

Mawaziri wa Tanzania na Vietnam waeleza mafanikio ya ziara ya Rais wa Vietnam nchini

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kueleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mhe. Truong Tan Sang. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.  
  Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietnam,  Mhe. Nguyen Bal Son akieleza kwa waandishi wa Habari nia ya Serikali ya Vietnam katika kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia hasa katika uchumi kwenye sekta ya Biashara,teknolojia na Viwanda ambapo ameiomba Serikali ya Tanzania kuainisha fursa zote za kiuchumi ili wananchi wa Vietnam waweze kuzitambua na kuja kuwekeza.
Balozi wa Tanzania nchini China  ambaye nawakilisha na Vietnam, Mhe. Balozi Abdulrahman Shimbo pamoja na Msaidizi wa Waziri Mahiga, Bw. Adolf Mchemwa wakifuatilia Mkutano.
Viongozi na Maafisa kutoka Serikali ya Vietnam wakifuatilia Mkutano.
Sehemu wa waandishi wakifuatilia Mkutano.
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano  ya Serikali na Wasemaji  katika Wizara za Mambo ya Nje kutoka nchini Tanzania, Bi. Mindi Kasiga (katikati)  na Vietnam Bw. Li Hai Bihn  (kushoto) pamoja na Mkalimani kutoka nchini Vietnam wakifuatilia Mkutano.
Mhe. Waziri Mahiga na Waziri Nguyen wakipongezana mara baada ya kumaliza Mkutano.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.