Mama Mai Thi Hahn akiwasalimia wanawake waliokuja kumlaki katika ofisi za Mhe. Mama Magufuli. |
Mama Mai Thi Hahn akisalimiana na mmoja wa wasanii wa vikundi vya ngoma vilivyofika kumlaki katika eneo la Ofisi za Mama Magufuli |
Mama Mai Thi Hahn akieleza umuhimu wa ziara yake na Mhe. Rais Toung Tang San ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi yake na Tanzania. |
Mama Magufuli akimkabidhi Mama Mai Thi Hahn zawadi ya Kinyago mashuhuri cha "Umoja" kilichochongwa nchini Tanzania. |
Pia Mama Mai Thi Hahn naye alikabidhi zawadi kwa Mama Magufuli. |
Wake za Marais wakicheza ngoma na kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza ofisini hapo. |
Mama Hahn na Mama Magufuli wakiagana na kina mama (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea ofisini
..........Alipotembelea Makumbusho ya Taifa |
Mama Hahn na Mama Magufuli wakisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa mara baada ya kuwasili. |
Mama Mai Thi Hahn akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi za Makumbusho za Taifa |
Mwenyeji wake Mama Janeth Magufuli naye akisaini kitabu cha wageni katika ofisi hizo. |
Wakiendelea kupokea maelezo. |
Wakielezewa na Afisa wa Makumbusho ya Taifa kuhusu picha zinazoonyesha historia ya utumwa ambapo wakati wa Ukoloni Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo watumwa walichukuliwa. |
Maelezo juu ya biashara ya pembe za ndovu enzi za ukoloni yakiendelea kutolewa. |
Mara baada ya kumaliza ziara hiyo Wake za Marais kwa pamoja walikabidhiwa zawadi ya vikapu vya asili na ofisi ya Makumbusho ya Taifa. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.