Thursday, March 10, 2016

Rais wa Vietnam atembelea Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA)

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Adelm Meru kwa Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang mara baada ya Rais huyo kuwasili Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa ajili ya kutembelea Mamlaka hiyo la uwekezaji na kujionea shughuli zinazofanywa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulishaMkurugenzi Mkuu wa EPZA, Mhe. Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Mwijage akimwelezea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong shughuli zinazofanywa na kampuni ya simu ya Halotel kutoka nchini Vietnam, ambapo alimwonyesha vocha za muda wa maongezi za mtandao huo ambazo zinapatikana katika gharama tofauti kulingana na nafasi ya kifedha ya myumiaji.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong akiongea na viongozi wa serikali ya Tanzania na Vietnam pamoja na wafanyabiashara katika Mkutano uliofanyika ukumbi wa ofisi za EPZA. Mhe Truong alieleza kuwa serikali ya Tanzania ijiandae kupokea wawekezaji wengi zaidi ya Kampuni ya Halotel kutoka nchini kwa kwake kupitia fursa za uwekezaji zilizopo katika Mamlaka hiyo ya EPZA. 

Mhe. Mwijage akiwasilisha taarifa ya Wizara juu ya fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania, hali halisi ya uwekezaji katika kituo cha EPZA na  jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuanzisha maeneo ya uwekezaji katika mikoa yote nchini kufuatia shughuli za kiuchumi zinazofaa katika Mkoa husika.

Mkurugenzi wa EPZA Kanali Mstaafu Mhe. Joseph Simbakalia akieleza hali ya uwekezaji katika kituo hicho ambacho kimegawanya maeneo ya uwekezaji katika kanda mbili, ambapo alisema kuna maeneo ya uwekezaji ya Serikali na binafsi pamoja na mikakati ya kuongeza  kanda nyingine za uwekezaji  sambamba na taarifa ya usimamizi wa kanda zilizopo.

Mkuruzenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Mbelwa Kairuki kulia akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Balozi Abdulrahman Shimbo anayewakilisha pia nchini Vietnam wakifuatilia mkutano uliokuwa ukiendelea.

Sehemu ya Maafisa wa EPZA waliohudhuria Mkutano wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa kutoka kwa viongozi

Sehemu ya Maafisa Waandamizi kutoka Vietnam na Tanzania wakiwa EPZA
Mhe. Mwijage akimkabidhi zawadi ya kinyago Mhe. Truong Tan Sang


Mhe. Truong naye alikabidhi zawadi ya picha ya maua kwa Mhe. Waziri ambapo alieleza ni maua yanayopendwa nchini Vietnam


Wakijadili jambo mara baada ya kumaliza Mkutano katika ofisi za EPZA Makao Makuu, Jijini Da es salaam, Pembeni ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Mkutano.




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.