Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC alikutana na Ujumbe wa JWTZ ulioongozwa na Mkuu wa Tiba Jeshini, Brigedia Jenerali (Dkt.) Denis Raphael Janga, aliyekuwa amefuatana na Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Tiba - Lugalo, Brigedia Jenerali (Dkt) Robinson Mboni Mwanjela.
Wengine ni Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wauguzi, Luteni Kanali Lawrence Tia Banda. Ujumbe huo ulikwa na ziara ya Kikazi ya wiki moja hapa Marekani, katika kuendeleza mahusiano baina na JWTZ na majeshi ya Marekani.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.