Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akimkaribisha Mhe. Philip Ruddock, Mjumbe Maalum wa Haki za Binadamu na Mwenyekiti wa Kamati ya pamoja ya Bunge nchini Australia, ambaye alimtembelea jana katika Ofisi za Wizara na kufanya naye mazungumzo.
Waziri Mahiga katika mazungumzo yake alieleza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Australia katika kuhakikisha inazisimamia na kuziwezesha Taasisi za Haki za Binadamu za hapa nchini na kuhakikisha haki hizo zinasimamiwa kikamilifu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia nafasi yake ya uenyekiti katika Jumuiya hiyo.
Mhe. Philip Ruddock naye alieleza nia ya wazi ya Australia kutaka kushirikiana kwa kufanya kazi pamoja na Serikali ya Tanzania katika Taasisi za Haki za Binadamu zilizopo nchini katika kuhakikisha haki za binadamu zinasimamiwa kikamilifu na changamoto zilizopo zinapata ufumbuzi mwafaka.
Ujumbe wa viongozi na Maafisa kutoka Ubalozi wa Australia nchini walioambatana na Mhe. Philip Ruddock wakifuatilia mazungumzo
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Eliet Magogo (kushoto) akiwa na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Ngusekela Nyerere nao wakifuatilia mazungumzo.
Wakiwa katika picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.