Saturday, June 11, 2016

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akutana na viongozi wakuu wa Kamisheni ya Utalii na Wanyamapori mjini Riyadh

Balozi Hemedi Iddi Mgaza akiwa Ofisini kwa Kiongozi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii ya Saudi Arabia, Mwanamfalme HRH Sultan bin Salman bin Abdulazizi kwenye mazungumzo ya ushirikiano.
Mhe. Balozi Hemedi Iddi Mgaza akipokea zawadi maalum ya kumbukumbu ya Utalii kutoka kwa Mwanamfalme HRH Sultan bin Salman bin Abdulazizi, Kiongozi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii ya Saudi Arabia.


Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza hivi karibuni alitembelea Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia mjini Riyadh na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mwanamfalme Bandar bin Muhammad Al-Saud. Aidha, alitembelea Kamisheni ya Utalii ya nchi hiyo na kukutana na Kiongozi mkuu wa Kamisheni hiyo Mwanamfalme Sultan bin Salman bin Abdul-Aziz. 


Mazungumzo ya Mhe. Balozi Mgaza na viongozi hao wawili yalilenga kuanzisha utekelezaji wa maeneo ya ushirikiano hususan katika sekta ya Maliasili na Utalii kwa mujibu wa Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia ambao ulisainiwa tarehe 23 Machi, 2016 mjini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.