Saturday, June 4, 2016

Mkoa wa Dar es Salaam wasaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Jimbo la JiangSu la nchini China


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Chama Tawala cha China Communist Party of China (CPC) Mhe. Luo Zhijun, ambaye jana alitembelea katika ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwekeana saini ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Mkoa huo na Jimbo la Jiangsu la nchini China 
Mhe. Makonda akihutubia wajumbe walioshiriki katika hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano (hawapo pichani) ambapo katika hotuba yake alieleza umuhimu wa Jiji la Dar es Salaam kiuchumi kwa taifa la Tanzania na fursa za uwekezaji zilizopo na kwamba lengo kuu la ushirikiano huo ni kupeana uzoefu katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili kuweza kukuza uchumi kwa mataifa yote mawili.
Mhe. Luo akizungumza katika hafla hiyo ambapo alieleza Tanzania na China zimekuwa na historia ya muda mrefu ya Ushirikiano hivyo kutokana na umuhimu wa Jiji la Dar es Salaam wameamua wameanze na Jiji hilo ili kuweza kuinua uchumi wa nchi ya Tanzania na  kwakua tayari Serikali na makampuni kutoka nchini China yameshawekeza miradi mikubwa iliyokwisha kamilika na inayoendelea kutekelezwa katika Jiji la Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Ramadhan Madabida akizungumza katika hafla hiyo, ambapo alieleza Tanzania ni nchi inayohitaji kujikwamua katika mambo makubwa matatu ambayo ni umasikini, ujinga na maradhi hivyo akasisitiza kuwa Chama tawala nchini Tanzania kipo tayari kutoa ushirikiano wa karibu kuhakikisha mahusiano yanayoanzishwa yanakuwa na tija ili kuweza kuinua maisha ya wananchi wake
Kushoto ni ujumbe ulioambatana na Mhe. Luo na kulia ni wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar e salaam pamoja na Viongozi wa chama wa Mkoa huo, kwa pamoja walishiriki katika hafla hiyo ili kuweza kushuhudia uwekaji saini wa makubaliano hayo
Kushoto ni Afisa Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Terezia Mmbando akiwa na wajumbe wengine kutoka katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na wale waliombatana na Mhe. Luo wakifuatilia hafla ili kuweza kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano
Mhe.Luo na Mhe. Makonda kwa pamoja wakiweka saini katika hati ya makubaliano ya ushirikiano.  
Wakifanya makabidhiano ya Hati mara baada ya kuwekeana saini
Katika hafla hiyo Mhe. Makonda alikabidhi zawadi ya kinyago cha faru kwa Mhe. Luo
Mhe. Luo pia alikabidhi zawadi ya picha kwa Mhe. Makonda

Wakijadili jambo mara baada ya hafla kumalizika


==================================================
Wakati huo huo ujumbe ulioambatana na Mhe. Luo pia ulitembelea Ofisi za Wizara ya Viwanda na Biashara na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Adelhelm Meru
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Adelhelm Meru akizungumza na ujumbe uliombatana na Mhe. Luo (hawapo pichani) katika mazungumzo yake aliwaeleza fursa za uwekezaji zilizopo katika nchi ya Tanzania, sambamba na kanda za kiuchumi za uwekezaji zilizoanzishwa na zinazoendelea kuanzishwa na kwamba wanakaribishwa kuja kuwekeza katika kanda hizo kwakua zimeandaliwa vizuri kwa lengo la kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika na uwekezaji huo
Mkuu wa msafara Bw. Chen Zhenning wa pili kutoka kushoto pia alieleza makampuni kutoka katika Jimbo la Jiangsu tayari yamekwisha wekeza katika nchi ya Tanzania katika ununuzi wa pamba, ujenzi wa barabara na Teknolojia ya mawasiliano hivyo kupitia ziara hii wataweza kuihamasisha jumuiya ya wafanyabishara kutoka katika Jimbo hilo kuja kuwekeza nchini Tanzania hasa katika viwanda ili kuweza kuendana na malengo ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli hasa katika kujenga Tanzania ya viwanda
Wakati mkutano ukiendelea 
 Bw. Chen Zhenning pia alimkabidhi Dkt. Meru zawadi ya picha

Mwenyekiti wa chama cha CPC akiwasili kutoka visiwani Zanzibar ambako pia alifanya ziara visiwani humo


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.