Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mkurugenzi wa Kanda wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji Bw. Jeffrey Labovitz alipotembelea Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji ametembelea nchini kwa mara ya kwanza toka shirika hilo lijiunge na Umoja wa Mataifa. Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili hali ya wakimbizi nchini, biashara haramu ya binadamu, hali ya wahamiaji haramu, na ushiriki wa watanzania wanaoishi ughaibuni katika kuchangia maendeleo ya nchi. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.