Tuesday, February 28, 2017
Monday, February 27, 2017
Wizara ya Mambo ya Nje yahamia Dodoma Rasmi
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU WIZARA KUHAMIA DODOMA
Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari
imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017. Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28
Januari, 2017 na awamu ya pili imetekelezwa
tarehe 17 Februari, 2017.
Miongoni mwa
Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza ni pamoja na Viongozi Wakuu
na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga na
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10)
waliofuatana nao.
Awamu ya
pili iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima na Naibu Katibu
Mkuu Balozi Ramadhan M. Mwinyi ambao waliongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Katika Uhamisho
huu, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu kwenye ofisi za
Makao Makuu ya Wizara na Serikali Dodoma.
Mawasiliano
ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa ni kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Barabara ya Makole,
S.L.P 2933,
Jengo la LAPF, Ghorofaya6,
DODOMA.
Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
Nukushi : +255-26-2323208,
Imetolewa na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 27 Februari, 2017.
Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa mkutano Ofisini Mjini Dodoma. |
Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Mahiga kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje kuhamia Dodoma. |
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha na baadhi ya watendaji wa Wizara mjini Dodoma. |
Sunday, February 26, 2017
Rais Museveni amaliza ziara yake nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini. |
Rais Museveni akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Innocent Shiyo. |
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Bw. Elibariki Maleko akiagana na Rais Museveni |
Rais Museveni akipunga mkono wa kwa heri kwa Rais Magufuli na Viongozi wengine walioshiriki kumuaga mara baada ya kumaliza ziara yake nchini. |
Rais Magufuli awaapisha mabalozi wanne
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Hazara Chana. Hafla za uapisho zimeanyika leo jijini Dar es Salaam |
Mhe. Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Chana |
Mhe. Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Silima |
Mhe. Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Kilima |
Mhe. Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Masuka |
Saturday, February 25, 2017
Tanzania yaahidi kuimarisha Diplomasia ya Uchumi na Uganda
Sehemu ya Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Serikali ya Tanzania waliohudhuria mkutano huo ambao ulitanguliwa na hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano katika masuala ya Siasa na Diplomasia. |
Wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini. |
Marais wakipongezana mara baada ya kutoa hotuba. |
Rais Museveni awasili nchini kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili
Rais Museveni pamoja na mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli wakisikiliza nyimbo za mataifa yao |
Makamu wa Rais akiwa uwanja wa ndege na Viongozi mbalimbali wa ngazi za juu Serikalini wakati wa mapokezi ya Rais Museveni. |
Rais Museveni pamoja na Rais Magufuli wakitizama moja ya kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani uwanjani hapo. |