TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU WIZARA KUHAMIA DODOMA
Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari
imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017. Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28
Januari, 2017 na awamu ya pili imetekelezwa
tarehe 17 Februari, 2017.
Miongoni mwa
Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza ni pamoja na Viongozi Wakuu
na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga na
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10)
waliofuatana nao.
Awamu ya
pili iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima na Naibu Katibu
Mkuu Balozi Ramadhan M. Mwinyi ambao waliongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Katika Uhamisho
huu, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu kwenye ofisi za
Makao Makuu ya Wizara na Serikali Dodoma.
Mawasiliano
ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa ni kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Barabara ya Makole,
S.L.P 2933,
Jengo la LAPF, Ghorofaya6,
DODOMA.
Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
Nukushi : +255-26-2323208,
Imetolewa na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 27 Februari, 2017.
Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa mkutano Ofisini Mjini Dodoma. |
Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Mahiga kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje kuhamia Dodoma. |
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha na baadhi ya watendaji wa Wizara mjini Dodoma. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.