Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Balozi Mteule wa Oman nchini, Mhe. Ali Abdullah Al Mahruqi alipomtembelea Wizarani leo, Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika masuala ya ushirikiano na juu ya ukamilishaji wa makubaliano ya kibiashara na uwekezaji ili kuweza kunufaika na ushirikiano wa kidiplomasia ambao umekuwa ukizidi kuimarika baina ya mataifa hayo mawili. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.