Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akizungumza mara baada ya kupokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe.Farhang. Kushoto ni Maafisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Iran nchini na Maafisa Kutoka Wizarani (kulia) wakifuatilia mazungumzo. Katika mazungumzo hayo Waziri alimkaribisha Balozi na kumhaidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezazi wa majukumu yake na kwa nchi ya Iran kwa ujumla, ili kuendeleza na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia uliodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Iran. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.