Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima (Kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuendeshea Mikutano kwa njia ya Video Wizarani Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Machi, 2017. Makabidhiano yanakamilisha sehemu ya vifaa vilivyotolewa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo ambavyo vilikabidhiwa tarehe 2 Februari, 2017 ili kuiwezesha Wizara kufanya kazi kwa ufanisi zaidi sambamba na kupunguza gharama za uendeshaji wa ofisi. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.