TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali
yamuondoa Mkurugenzi wa UNDP nchini
Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania imeliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa la Programu ya
Maendeleo (United Nations Development Programs – UNDP) kwa upande wa Tanzania
kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi Awa Dabo.
Serikali ilifikia
uamuzi huo kutokana na Bi Dabo kutokuwa
na maelewano mazuri na baadhi ya Watumishi wenzake na Menejimenti ya Shirika
hilo, hivyo kupelekea kuzoretesha utendaji wa shirika hilo nchini na kupunguza
kasi ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka
zisingechukuliwa.
Baada ya
kuthibitishiwa kuondoka nchini, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imetoa
rai kwa UNDP kuwakumbusha Watumishi wake kuwa kipaumbele chao ni kufanya kazi
na Serikali ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya
Mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na Malengo ya Maendeleo
Endelevu ambayo yamefafanuliwa katika Agenda ya Mwaka 2030.
Mwisho.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasili ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma,
25 Aprili 2017.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.