Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefikia tamati leo Ikulu Jijini Dar es Salaa. Mkatano huu ulikuwa na ujumbe na uwakilishi kutoka nchi zote sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki. .
Rais Mhe. Dkt. Magufuli akizungumza katika Mkutano huu wakati wa kukabidhi kiti cha Uwenyekiti amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Uwenyekiti wa Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata mafanikio makubwa na kuifanya istawi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara kutokana na kupunguzwa kwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiforodha, kuboreka kwa mfumo wa elimu ya Juu ndani ya Jumuiya na kuongezeka kwa Sudan Kusini katika Jumuiya.
Aidha mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Mhe. Museveni akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo amesema kunakila sababu ya kulinda na kudumisha Mtangamano kwa kuwa unaharakisha kasi ya maendeleo ya nchi wanachama na watu wake, unaimarisha ulinzi na usalama wa nchi wanachama, na kudumisha undugu wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu miongoni mwa nchi wanachama.
Pia Mkutano huu wa 18 wa Wakuu wa nchi umeshuhudia viapo vya viongozi wapya wawili katika ngazi ya Jumuiya ambao ni Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Jaji Charles Oyo Nyawezo na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Eng. Steven Mrote kutoka Tanzania.
Katika Kutano huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhi rasmi uwenyekiti kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni.
|
Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia hadhira iliyohudhuria Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaa. |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini moja ya nyaraka ya makabidhiano ya uwenyekiti wakati wa Mkutano wa 18 wa Kaiwa wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mshariki. |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.