TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Siku ya Kongamano la Biashara ya Kilimo na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uholanzi yafana
Katika
kutekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi, Ubalozi wa Tanzania kwa kushirikiana na
Ubalozi wa Uholanzi uliopo Tanzania, Wizara ya Masuala ya Uchumi na Wizara ya
Mambo ya Nje za Uholanzi na Taasisi ya Netherlands–African
Business Council (NABC)kwa pamoja ziliandaa Kongamano la Biashara na
Uwekezaji lililofanyika hapa The Hague, Uholanzi tarehe 31 Mei 2017. Lengo kuu
la Kongamamo hilo, pamoja na kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo kati ya
Tanzania na Uholanzi, nikutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji
zilizopo nchini Tanzania hususan katika Sekta za Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Miundombinu
ya Kilimo. Aidha, Kongamano hilo lililohudhuriwa na Wawakilishi wa Makampuni
takriban mia moja (100) ni mwendelezo wa utekelezaji wa makubaliano
yaliyofikiwa kwenye Mkataba kati ya Tanzania na Uholanzi kuhusu Uingizwaji wa
Mbegu za Viazi kutoka Uholanzi uliosainiwa kwenye ziara ya Mhe. Martijn Van
Dam, Waziri wa Kilimo wa Uholanzi nchini Tanzania tarehe 16 Juni 2016. Aidha,
Kongamano hii lilitanguliwa na ziara ya ujumbe kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo
mashamba yanayomilikiwa na wakulima na wafugaji binafsi nchini Tanzania pamoja
na kupata fursa za kusikiliza mada mbalimbali zilizotolewa na wakulima/wafugaji
na wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Wageningen
kinachohusika na kufanya tafiti za Kilimo na Ufugaji.
Ujumbe
kutoka Tanzania uliongozwa na Mhe.Eng. Mathew Mtigumwe, Katibu Mkuu
anayeshughulikia Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi,
akimwakilisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Wajumbe
wengine ni:
ü Mhe.
Yohana Budeba, Katibu Mkuu anayeshughulikia Uvuvi, Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi,
ü Mhe.
Irene F.M. Kasyanju, Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi,
ü Bw.
Twahir Nzallawahe, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao, Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi,
ü Bibi
Anuciata Njombe, Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Mifugo na Masoko, Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi,
ü Bw.
Geoffrey Kirenga, Mtendaji Mkuu wa Kituo cha kuendeleleza Kilimo Ukanda wa
Kusini (SAGCOT),
ü Bibi
Jennifer Baarn, Naibu Mtendaji Mkuuwa Kituo cha kuendeleleza Kilimo Ukanda wa
Kusini (SAGCOT),
ü Professa
Andrew Temu, Mkurugenzi wa Diligent Consulting
Ltd na Mwanachama wa Bodi ya SAGCOT,
ü Bibi
Jacqueline Mkindi, Mtendaji Mkuu wa Tanzania
Horticulture Association (TAHA),
ü Bw.
Hussein Sufiani Ally, Mkurugenzi wa AZAM
Bakhresa Group,
ü Bibi Mona Mahecha, Afisa Mambo ya
Nje Mwandamizi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
ü Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania
Uholanzi Bw. Matiku Kimenya (MC), Bibi Naomi Z. Mpemba (CO) na Bibi Agnes K.
Tengia (FS).
Kwa
upande wa Serikali ya Uholanzi, ujumbe uliongozwa na Mhe. Bibi Marjolijn
Sonnema, Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kilimo, Wizara ya Masuala ya
Uchumi ya Uholanzi ambaye pia anakaimu kama Naibu Waziri wa Kilimo. Wengine ni;
ü Mhe.
Jaap Fredericks, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania,
ü Bw.
Bert Rikken, Afisa anayeshughulikia Masuala ya Kilimo, Ubalozi wa Uholanzi
nchini Tanzania/Kenya,
ü Bibi
Ingrid Korving, Afisa Sera Mwandamizi, Wizara ya Masuala ya Uchumi ya Uholanzi,
ü Bibi
Hennie Wellen, Mratibu Wageni wa Kimataifa, Wizara ya Masuala ya Uchumi ya Uholanzi,
ü
Bibi Theresia Mcha, Afisa Kilimo,
Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania.
Katika
Kongamano hili, Viongozi wa Ujumbe wa Serikali ya Tanzania na Uholanzi
walionesha dhamira ya kuendelea kushirikiana kwa pamoja kwa kusaini Barua (Letter of Intent) ya kuanzishwa kwa
Kituo cha Kuendeleza Zao la Viazi nchini Tanzania (Centre for Development of the Potato Industry in Tanzania- CD PIT).
Aidha, Makampuni takriban kumi (10) yanayojishughulisha na kilimo cha viazi, yalionesha
utayari wa kuwa wanachama kwa kushirikiana na Serikali za nchi hizi mbili
katika uanzishwaji wa Kituo hicho. Tukio hilo lilikamilishwa kwa Wawakilishi wa
Makampuni hayo kuweka saini kwenye Kadi/Bango kuonesha utayari wao.
Kituo
cha CD PIT kinatarajiwa kuanzishwa
Mkoani Mbeya ambapo pamoja na kukuza maendeleo ya sekta binafsi na kutoa ajira,
kitatoa mafunzo ya kujenga uwezo hususan katika uzalishaji na utafutaji masoko,
kitaendesha tafiti mbalimbali za kilimo ikiwemo pia kukuza uhusiano wa
kibiashara kati ya Tanzania na Uholanzi.
Ubalozi
kwa upande wake umeridhishwa na mwitikio mkubwa uliooneshwa na wadau mbalimbali
waliojitokeza kushiriki katika Kongamano hilo. Hii inadhihirisha kuzidi
kuimarika kwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi mbili.
Pamoja
na kubadilishana uzoefu, kujifunza na kufahamiana, Kongamano hilo liliwezesha
wadau kupata fursa ya kujadili pia changamoto wanazokabiliana nazo katika
shughuli mbalimbali za biashara na uwekezaji wanazoziendesha nchini Tanzania.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
The Hague, Uholanzi, 09
Juni 2017
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.