Friday, July 14, 2017

Vijana wahimizwa kuchangamkia fursa katika boda za EAC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga akiwahutubia vijana kwenye kongamano la kuwahimiza kuchangamkia fursa za biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, hususan mipakani. Kongamano hilo lenye kaulimbiu "Chungulia Fursa Border to Border limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Taasisi ya Sekta Binafsi  na Trade Mark East Afrika ambao ni wafadhili wakuu wa kongamano hilo. Kongamano litafanyika kwa siku 10 katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Mwanza na Arusha.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed akiwasilisha hotuba katika kongamano hilo. Waziri Mohammed alisema lazima vijana wapewe fursa kwa kuwa wao ndio nguzo ya usalama na amani kwenye Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, alisema wao ni waanzilishi tu lakini uhai wa Jumuiya unategemea vijana namna watakavyoilinda na kuidumisha jumuiya hiyo.

Waziri Mohammed akiendelea kusoma hotuba yake kwa vijana wanaoshiriki kongamano hilo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa na washiriki wa kongamano la kuhamisha vijana kuchamkia fursa za EAC

Mkurugenzi Mkazi wa East Africa TradeMark, Bw. John Ulanga ambaye taasisi yake ni mdhamini wa kongamano hilo akieleza majukumu ya taasisi hiyo katika kutoa elimu ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga (katikati) akizindua moja ya kitabu cha tafiti zilizofanywa na REPOA kuhusu ajira na ushiriki wa Asasi za kijamii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wengine kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa TMEA na Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Sekta Binafsi

Washiriki wa kongamano wakionesha mshikamano ambao wataenda nao katika kuchamkia fursa za EAC

Burdani



Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya awasilisha Ujumbe Maalum
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Amina Mohammed. Mhe. Mohammed amekuja nchini kwa ziara ya siku moja kwasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Kenya, Mhe Uhuru Kenyatta kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt, John Pombe Magufuli. Mawaziri hao wamekubaliana na pendekezo la kuunda Kamati ambayo itaongozwa na wao wenyewe itakayokuwa na jukumu la kushughulikia kwa haraka matatizo ya kibiashara yatakayojitokeza kati ya nchi hizo.

Ujumbe wa Tanzania na Kenya ukiwa katika mazungumzo

Waziri Mahiga akipokea Ujumbe Maalum kwa niaba ya Mhe. Rais Magufuli kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya
Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.