Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid (kulia) akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania, Bw. Saleh Kusa Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam leo. Wawili hao walijadili namna ya kukamilisha taratibu za kukabidhi msaada wa matrekta 10 yenye thamani ya zaidi ya milioni 250 za Tanzania kutoka Libya kwa ajili ya Serikali ya Zanzibar. Matrekta hayo yashawasili jijini Dar es Salaam na wiki ijayo yanatarajiwa kukabidhiwa Serikali ya Zanzibar. Aidha, Kaimu Balozi alisema kuwa Libya imetenga Dola Bilioni 20 kupitia Mfuko wa "Libyan-Africa Investment Portfolio" kwa ajili ya nchi za Afrika. Aliahidi kuwa atahakikisha kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zinaletwa Tanzania. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.