Thursday, September 21, 2017

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki (Mb.), akitoa Salamu za pole kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa familia, ndugu na jamaa wote waliofiwa na ndugu zao kutokana na ajali iliyotokea Nchini Uganda, pia alitumia fursa hiyo kutoa neno la shukrani kwa Serikali ya Uganda kwa kusaidia kusafirisha miili ya ndugu zetu kuja nchini Tanzania kwa taratibu za mazishi, Serikali ya Uganda imewakilishwa na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Masuala ya Jiji la Kampala Mhe. Betty Namisango na  Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe. Balozi Richard Kabonelo


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba(wa pili kutoka kushoto), Profesa Charles Ibingira baba wa bwana Harusi(Kulia kwake), Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu ( wa mwisho kulia) na Dkt Gregory Teu baba wa bibi harusi ( wa mwisho kushoto)wakiwa na majonzi katika shughuli ya kuaga miili ya watanzania waliopoteza maisha

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga akitoa utaratibu kwenye tukio la kuaga miili ya watanzania waliopata ajali nchini Uganda.
Sehemu ya Ndugu waliofiwa wakiwa na nyuso za huzuni.
Miili ya Watanzania waliopata ajali nchini Uganda ikiwasili
Viongozi mbalimbali wa Serikalini wakiongozwa na Mhe. Angela Kairuki wakiwa wamesimama kwa pamoja wakati miili ya watanzania waliopoteza maisha ikiwasili.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.