Thursday, December 14, 2017

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ampokea Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi wakipita kwenye gadi ya heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati Rais huyo akiwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma

Vikundi vya ngoma za jadi vikisherehesha katika shughuli za mapokezi ya Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi wakati akimpokea mjini Dodoma. Rais Nyusi amewasili leo mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli, kabla ya kuelekea Ofisini kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao wamejadili na kukubaliana masuala mbalimbali ya kukuza na kuendeleza ushirikiano uliodumu kwa muda mrefu baina ya Mataifa haya mawili (Tanzani na Msumbiji). Aidha Rais Magufuli na Rais Nyusi wamekubaliana kuanzisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo katika sekta ya gesi usafiri wa anga na miundombinu.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi alipowasili uwanja wa ndege wa mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja


        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.               Dkt.  John Pombe Magufuli  akiwa na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi katika Ikulu ndogo ya Mjini Dodoma kabla ya kuanza mazungumzo yao

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.