Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni na Wajumbe wa Baraza la Wakimbizi Duniani. Hafla hiyo iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuhudhuriwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne na Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Wakimbizi Duniani, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wakimbizi Duniani Mhe. Lloyd Axworthy, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Balozi Simba Yahaya (hawapo pichani). Hafla hiyo imefanyika katika Hotel ya Hyatt Regancy, Jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.