Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga akiwa katika mkutano na Mabalozi kutoka Umoja wa Ulaya na Marekani wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Wizara, Dar es Salaam, tarehe 9 Februari,2018.
Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Waheshimiwa Mabalozi waliishukuru Tanzania kwa mchango mkubwa inaoutoa katika kutatua mgogoro wa Burundi na Congo, pia wametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kusaidia juhudi za kutatua migogoro hiyo kwani wanaamini Tanzania ina mchango mkubwa katika kutafuta utatuzi wa kudumu wa migogoro hiyo ili nchi hizi kujikita zaidi katika shughuli za kujiletea maendeleo.
Sehemu ya Waheshimiwa Mabalozi wakifuatilia Mkutano huo
Mheshimiwa Waziri akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Mabalozi, kushoto mbele ni Balozi Grace Mujuma, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika na kulia mbele ni Bw. Joseph Kapinga, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akizungumza na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini walipomtembelea Wizarani, Dar es Salaam tarehe 9 Februari,2018.
Katika mazungumzo hayo walizungumzia jinsi ya kuboresha zaidi mahusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na pia kuangalia jinsi Umoja wa Ulaya unavyoweza kuendelea kusaidia Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani Umoja wa Ulaya ni kati ya wadau muhimu wanaochangia miradi mbalimbali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, Wajumbe hawa kwa upande wao walisifia Serikali ya awamu ya 5 inavyotekeleza miradi mbalimbali inayowagusa moja kwa moja wananchi, pia walisifia muongozo wa utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali katika Idara mbalimbali za Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi ( Blue Print) na kusema utakapokamilika itakuwa ni njia nzuri ya kutekeleza kwa haraka masuala mablimbali ya Serikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda na Wajumbe kutoka Umoja wa Ulaya hapa nchini pamoja na Maafisa wa Wizara wakiendelea na mazungumzo.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika Balozi Grace Mujuma,akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi msaidizi wa Masuala ya Afrika katika Wiazara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi ambaye pia ni Mjumbe maalum wa Ukanda wa Maziwa Makuu (Great Lakes Region), Bw. Robert - Jan Siegert alipomtembelea Wizarani tarehe 9 Februari,2018, Wengine katika Picha ni Naibu Balozi wa Uholanzi Bibi Lianne Houben, na Maafisa kutoka Ubalozi wa Uholanzi na wa kwanza kulia ni Bw. Ally Ubwa Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizarani.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.