Waziri Wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum akizungumza katika ufunguzi wa mkutano na Wafanyabishara wa Zanzibar uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko tarehe 13 Aprili 2018. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Katibu wa Kamati ya Taifa ya maandalizi ya maonesho ya bidhaa za Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega.
Katika ufunguzi huo Mhe. Waziri Amina aliwasisitiza wafanyabiashara hao kushiriki katika maonesho pamoja na umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.