TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
FURSA
ZA UFADHILI WA MAFUNZO KWA WATANZANIA
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda
mfupi na muda mrefu katika kada mbalimbali kutoka Umoja wa Afrika, Serikali za China,
Ujerumani na Jamhuri ya Korea.
Kuhusu ufadhili wa mafunzo ya muda
mrefu, Umoja wa Afrika kupitia Mwalimu
Nyerere African Union Scholarship Scheme umetoa ufadhili wa mafunzo kwa
ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu (PhD) kwenye masuala ya Sayansi,
Teknolojia, Uhandisi na Hesabu (STEM). Waombaji wa mafunzo haya ni wanawake
pekee wenye umri wa miaka isiyozidi 35 kwa mafunzo ya ngazi ya Shahada ya Uzamili
na miaka isiyozidi 40 kwa mafunzo ya ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD). Maelezo
ya ziada kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia tovuti ya http://www.au.int. au maombi yatumwe kwa OlgaA@african-union.org na nakala
kwa mwalimunyerere@africa-union.org. Mwisho
wa kutuma maombi ni tarehe 30 Aprili, 2018. Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma.
Aidha, Baraza la Ufadhili wa
Mafunzo la China limetoa nafasi za ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu. Maelezo
kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia http://www.esc.edu.cn. Mwisho
wa kutuma maombi ni tarehe 30 Aprili, 2018. Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora.
Vilevile, Serikali ya China imetoa fursa ya ufadhili wa
mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili katika masuala ya Utawala
na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Nadharia ya Uchumi na Maendeleo ya Taifa.
Maelezo ya ziada ya kozi hizi yanapatikana kupitia http://www.isscad.pku.edu.cn. Pia
maombi yatumwe kupitia http://www.administration@isscad.pku.edu.cn. Mwisho
wa kutuma maombi ni tarehe 30 Mei, 2018. Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa pamoja na Ofisi ya Rais, Menejimentii ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Wakati huohuo, Serikali ya China
imetoa fursa za ufadhili wa mafunzo kwa wataalam wa kilimo kutoka Tanzania.
Mafunzo haya yatafanyika Beijing, China. Mratibu wa mafunzo haya ni Wizara ya
Kilimo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kwa upande mwingine, Wizara
imepokea nafasi za mafunzo ya muda mfupi kutoka Serikali ya Ujerumani katika
Kozi ya Stashahada ya Juu ya Usimamizi wa Mazingira kwa Nchi Zinazoendelea (International Postgraduate Course on
Environmental Management for Developing Countries). Mafunzo haya
yatafanyika Ujerumani kuanzia tarehe 10 Januari, 2019 hadi tarehe 12 Julai,
2019. Mafunzo haya yanaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira) na
Baraza la Mazingira (NEMC).
Pia, Jamhuri ya Korea kupitia
Program ya Dkt. Lee Jong-Wook imetoa nafasi mbili za ufadhili wa masomo ya muda
mfupi kwa wataalam wa tiba kwa kipindi cha kati ya miezi 2 hadi 12. Mafunzo
haya yanaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
06 Aprili, 2018
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.