Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Chris Kiptoo ambaye pia ni mgeni rasmi katika kongamano hilo la biashara akitoa hotuba ya ufunguzi wa ambapo alieleza kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza mzunguko wa biashara baina ya Tanzania na Kenya pia ni wakati mwafaka wa kutumia fursa za rasilimali zilizopo baina ya mataifa hayo.
|
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akihutubia katika ufunguzi wa kongamano la biashara ambapo alieleza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kufanya biashara na Jamhuri ya Kenya na kwamba maadhimisho ya kipekee ya wiki ya Tanzania nchini Kenya ni mwanzo wa kuimarisha na kuboresha ushirikiano uliopo na hivyo akasisitiza ni vema uma wa mataifa haya mawili ukajielekeza katika kununua na kuuza bidhaa baina yao. |
|
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na uhamasishaji na mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF), Bi Neema Temba akitoa neno la utangulizi katika kongamano la biashara ambapo alisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kuwa na ushindani unaojenga baina yao na pia alieleza sekta binafsi ni vizuri ikatambua na kuunga mkongo jitihada za serikali katika kuweka mazingira wezeshi ya biashara. |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.