Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Mhe. Prof. Jacek Czaputowicz mara baada ya kumkaribisha rasmi Wizarani tarehe 12 Aprili, 2018. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo elimu, kilimo, utalii, biashara na uwekezaji. Mhe. Czaputowicz yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atazindua rasmi ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.