Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda, akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria kikao baina yake, watendaji wa Kituo hicho na wafanyabiasha wanaozunguka eneo hilo kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo.
Pro. Mkenda katika ziara hiyo aliambatana na Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya.
Wawili hao kwa pamoja sambamba na kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho katika pande zote mbili za Tanzania na Kenya walipata fursa ya kuongea na watendaji wanaohudumu katika kituo hicho.
Lengo la ziara hii ilikuwa nikuangalia ufanisi wa kituo hicho katika kusaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kutika pande zote mbili za Tanzania na Kenya hivyo kurahisisha shughuli za biashara.
Vilevile ziara hii ililenga kubaini changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho na kupelekea kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi wanaotumia kituo hicho.
Aidha Makatibu Wakuu hao wamezipongeza Mamlaka na Taasisi zote zilizopo katika kituo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.